Zaidi ya wanafunzi 280 watekwa nyara Nigeria
8 Machi 2024Matangazo
Maafisa wa serikali katika jimbo la Kaduna wamethibitisha utekaji nyara huo katika shule ya Kuriga hapo jana, ila hawakutoa idadi kamili. Mmoja wa walimu katika shule hiyo iliyoko mkoa wa Chikun Sani Abdullahi, amesema walimu walifanikiwa kutoroka na wanafunzi wengi wakati wavamizi hao walipokuwa wakifyatua risasi hewani. Mkaazi wa eneo hilo Mohammad Adam ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba, zaidi ya watoto 280 ndio waliotekwa nyara baada ya kufanya hesabu kwa umakini zaidi. Kwa kawaida idadi ya waliotekwa nyara Nigeria hurudi chini baada ya waliokimbia uvamizi kurudi makwao.