Niger, Mali na Burkina Faso zatangaza kujiondoa ECOWAS
28 Januari 2024Matangazo
Viongozi wa mataifa hayo matatu ya ukanda wa Sahel walitoa taarifa ya pamoja wakisema ni "uamuzi huru" kujiondoa katika jumuiya hiyo "bila kuchelewa".
Katika taarifa hiyo msemaji wa jeshi la Niger, Kanali Amadou Abdramane, amesema jumuiya ya ECOWAS imeshindwa kuyasaidia mataifa hayo katika mapambano yao dhidi ya ugaidi na ukosefu wa usalama.
Aidha taarifa hiyo imeishutumu ECOWAS, kwamba iko chini ya ushawishi wa mataifa ya kigeni, kusaliti misingi ya kuanzishwa kwake, na kuwa imekuwa tishio kwa wanachama wake na watu wake ambao inapaswa kuhakikisha kuwa wana furaha.
Niger, Mali na Burkina Faso zilisimamishwa uanachama na jumuiya hiyo huku Niger na Malizikikabiliwa na vikwazo vikali.