Mali yauonya Umoja wa Mataifa dhidi ya Uingiliaji Niger
24 Septemba 2023Diop aliyewakilisha utawala wa kijeshi wa Mali katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa, amesema kuwa Mali bado inapinga vikali uingiliaji wowote wa kijeshi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS, na kwamba uvamizi wowote nchini Niger unatoa tishio la moja kwa moja kwa amani na usalama wa Mali na hata kwa ukanda huo, hatua aliyosema italeta madhara makubwa.
Diop aikosoa Ufaransa
Diop amesema haya baada ya jeshi la mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso kusaini wiki iliyopita mkataba wa pamoja wa ulinzi.
Soma pia:Viongozi wa kijeshi wa Niger wamkosoa Guterres
Wakati wa kikao hicho cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Diop aliikosoa Ufaransa kwa kile alichosema ni utawala unaojikita katika ukoloni mamboleo huku akiusifia ushirikiano na Urusi.