1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Burkina Faso yalifungia gazeti la kifaransa la Jeune Afrique

26 Septemba 2023

Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso umelisimamisha gazeti la lugha ya kifaransa la Jeune Afrique kwa madai ya kuchapisha ripoti za uongo zilizoibua wasiwasi na sintofahamu kwenye majeshi ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4WnmP
Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Ibrahim Traore aliposhiriki moja ya sherehe za kitaifa mjini Ouagadougou, Oct. 15, 2022. Utawala wake umekuwa mkali dhidi ya gazeti la kifaransa la Jeune Afrique na kuliadhibu vikali
Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Ibrahim Traore aliposhiriki moja ya sherehe za kitaifa mjini Ouagadougou, Oct. 15, 2022. Utawala wake umekuwa mkali dhidi ya gazeti la kifaransa la Jeune Afrique na kuliadhibu vikaliPicha: Kilaye Bationo/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana jioni imelishutumu gazeti hilo kwa kutaka kulidhalilisha jeshi na kusambaza habari ili "kueneza machafuko" nchini humo, likiangazia makala mbili zilizochapishwa na gazeti hilo siku nne zilizopita.

Hii ni moja ya hatua kali za karibuni kali zinazochukuliwa dhidi ya gazeti hilo la kifaransa, tangu utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso ulipoingia mamlakani, huku uhusiano kati ya mataifa hayo ukizidi kudhoofika.

Jeune Afrique halikuzungumza chochote lilipoombwa kuzungumzia uamuzi huo unaochukuliwa miezi minane tangu Kapteni Ibrahim Traore alipoingia madarakani kufuatia mapinduzi ya Burkina Faso.