1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paundi milioni 300 kuwahamishi wakimbizi Rwanda

1 Machi 2024

Mpango wenye utata wa Uingereza kuwahamishia waomba hifadhi nchini Rwanda huenda ukagharimu zaidi ya pauni milioni 600 kwa wakimbizi 300.

https://p.dw.com/p/4d5Wa
Wakimbizi Uingereza
Wakimbizi wakivuuka ujia wa maji kutokea Ufaransa kuingia Uingereza mwezi Agosti 2023.Picha: Jordan Pettitt/PA Wire/empics/picture alliance

Hayo yalisemwa siku ya Ijumaa (Machi 1) na ofisi inayosimamia matumizi ya fedha bungeni nchini Uingereza.

Kulingana na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAO), mbali ya pauni 220 ambazo tayari Uingereza imeshailipa Rwanda, serikali imekubali kulipa paundi milioni 150 nyengine katika miaka mitatu ijayo.

Soma zaidi: UN yaelezea wasiwasi wake kuhusu mpango wa Uingereza kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Vile vile, Uingereza itailipa Rwanda pauni milioni 120 mara tu baada ya waomba hifadhi 300 wa kwanza kupewa hifadhi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Serikali ya Uingereza pia italazimika kuilipa Rwanda zaidi ya pauni 150,874 kama  gharama za kila mmoja atakayepata makaazi mapya.

Soma zaidi: Baraza la juu la Bunge la Uingereza lapiga kura kuchelewesha mpango wa Sunak

Pamoja na gharama za nauli ya kuwahamisha, shirika hilo limekadiria jumla ya fedha zitakazotumika kuwa zaidi ya pauni milioni 600.

Mchakato wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda ungali unakumbwa na visiki.