1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN inamashaka ya mpango wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda

20 Februari 2024

Mkuu wa Shirika la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk, ameelezea wasiwasi wake kuhusu kufufuliwa kwa mpango wa Uingereza wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda.

https://p.dw.com/p/4ccns
Volker Türk
Mkuu wa Shirika la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: KHALED DESOUKI/AFP

Turk amesema hatua hiyo itakuwa sawa na kuinyakua Mahakama uwezo wake wa kutathmini maamuzi ambayo yanaweza kuwa hatari na pigo kubwa kwa haki za binaadamu, huku akikumbushia uamuzi uliotolewa na Mahakama za Uingereza zilizopinga mpango huo kwa kusema Rwanda si nchi salama.

Sunak apata "pigo" katika kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Waziri Mkuu Rishi Sunak anajaribu kupitisha mpango huo kupitia bunge ambalo litaitambua Rwanda kuwa nchi salama kwa wahamiaji hao, licha ya mashaka kutoka kwa baadhi ya wabunge ambao wanapinga mpango huo na kuutaja kutokuwa wa kimaadili na usiotekelezeka.

Tangu kuanza kwa mwaka huu, zaidi ya wahamiaji 1,300 wamewasili Uingereza kwa kutumia mashua ndogo.