Bunge Uingereza lauchelewesha mpango wa wakimbizi wa Sunak
23 Januari 2024Matangazo
Hatua hiyo ni pigo kubwa kwa Waziri Mkuu Rishi Sunak, aliyeliomba baraza hilo kuupitisha mpango huo, akisema ndio matakwa ya Waingereza walio wengi.
Kura 214 kati 171 zilipigwa kuuchelewesha mpango huo uliotiwa saini kati ya Uingereza na Rwanda, hadi pale serikali ya Uingereza itakapoonesha na kwamba Rwanda ni mahala salama kwa wahamiaji watakaoondolewa kutoka Uingereza.
Soma pia: Sunak apata "pigo" katika kuwapeleka wahamiaji Rwanda
Mpango huo ni muhimu kwa serikali ya kihafidhina ya Rishi Sunak, kudhibiti uhamiaji haramu, kwa kuwapeleka waomba hifadhi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.