1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kaimu Mkuu wa polisi Kenya ahukumiwa miezi 6 jela

13 Septemba 2024

Kaimu mkuu wa polisi wa Kenya, Gilbert Masengeli, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela. Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa kufuatia hatua ya Masengeli kukaidi mara kadhaa maagizo ya kumtaka afike kortini.

https://p.dw.com/p/4kc9n
Jengo la Mahakama Kuu Kenya
Jengo la Mahakama Kuu KenyaPicha: John Ochieng/SOPA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Kortini ilimtaka afisa huyo kutoa maelezo kuhusu wapi waliko wanaume watatu wanaodaiwa kutekwa nyara na maafisa wa polisi.

Jaji katika kesi hiyo alikuwa ameahirisha kutoa uamuzi kwa siku saba ili kumpa Masengeli nafasi ya mwisho kufika kortini kabla ya hukumu kutolewa.

Soma pia:Vyombo vya usalama vya Tanzania vyalaumiwa kwa mauaji

Hukumu hiyo inatokana na kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Kenya kutaka mahakama itoe agizo la kuachiliwa na kufikishwa mahakamani watu watatu waliokamatwa na polisi mwezi Agosti na hadi sasa hawajaonekana wala kusikika.