1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa mazingira - COP29 waanza Azerbaijan

11 Novemba 2024

Mkutano wa kilele wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira, COP29, unaanza nchini Azerbaijan huku nchi zikijiandaa kwa mazungumzo magumu kuhusu fedha na biashara.

https://p.dw.com/p/4mruk
Azerbaijan - BAKU  COP29
Ajenda kuu ya mkutano wa COP29 ni upatikanaji wa dola trillioni 1 katika ufadhili wa kila mwaka kwa ajili ya nchi zinazoendelea.Picha: Alexander Nemenov/AFP

Mkutano huo unafanyika baada ya mwaka mmoja wa majanga ya hali ya hewa ambayo yamezipa matumaini nchi zinazoendelea katika madai yao ya ufadhili wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Wajumbe kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni, wanakusanyika katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku, wakitumai kupata mwafaka wa ajenda kuu ya mkutano wa COP29ya upatikanaji wa dola trillioni 1 katika ufadhili wa kila mwaka kwa ajili ya nchi zinazoendelea. Lengo hilo limo mashakani kufikiwa kutokana na wasiwasi wa kiuchumi, vita vya Gaza na Ukraine na kuchaguliwa tena kwa Donald Trump.