MINUSMA waanza kuondoka Mali
17 Oktoba 2023Matangazo
Hatua inayoanzisha awamu mpya ya kulazimishwa kuondoka ambayo inaibua hofu kwamba mapigano yataongezeka kati ya wanajeshi wa Mali na makundi yenye silaha.
Soma zaidi: Watu 64 wauawa nchini Mali katika mashambulizi mawili tofauti
Kikosi hicho cha amani cha Umoja wa Matiafa kinachofahamika kama MINUSMA kilitarajiwa kuondoka kutoka kambi zake katikati ya Oktoba lakini kikaahirisha wakati eneo hilo lililopokabiliwa na ongezeko la machafuko na mapigano.
Soma zaidi: Awamu ya pili ya kuwaondoa walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali "itakuwa ngumu"
Kwa mujibu wa maafisa wawili wa uwanja wa ndege, jeshi la Mali limetuma ndege mbili katika kambi ya Tessalit zikiwabeba vikosi vya wanajeshi na wapiganaji wa kundi la mamluki la Wagner kutoka Urusi.