Meloni; Tushirikiane kudhibiti wimbi la wahamiaji Ulaya
24 Julai 2023Akizungumza jana Jumapili katika Mkutano wa kilele wa Kimataifa wa Maendeleo na Uhamiaji uliofanyika mjini Roma na kuzihusisha takribani nchi 20, Meloni amesema ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya mataifa ili kukabilianana wimbi la wahamiaji wanaoingia Ulaya kwa msaada wa Afrika.
Mkutano huo unakusudia kuifanya Italia kuwa kiongozi katika kutatua masuala yanayoathiri mataifa yaliyoko katika Bahari ya Mediterania.
Soma pia:Meloni: Ushirikiano mkubwa unahitajika kukabiliana na wahamiaji wanaoingia Ulaya
Jambo kuu miongoni mwake ni uhamiaji, kwani Italia inawahifadhi mamia ya wahamiaji wapya wanaowasili kila siku kwenye mpaka wa kusini mwa Ulaya, lakini pia nishati, huku Ulaya ikiitazama Afrika na Mashariki ya Kati kama zitakazochukua nafasi ya kudumu ya usambazaji wa Urusi.
Meloni amesema kuna uwezekano kuwa kiburikinachoonyeshwa na mataifa ya Magharibi, kimekuwa kikwazo katika kutafuta suluhisho la suala la uhamiaji.