Mawaziri wa EU wajadili mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine
30 Agosti 2024Matangazo
Mawaziri hao pia watajadiliana mpango wa kuzihamishia operesheni hizo za mafunzo ndani ya Ukraine, tofauti na Poland na Ujerumani ambako mafunzo hayo yanafanyika kwa sasa.
Ufaransa na Lithuania zimeashiria kuunga mkono hatua hiyo, licha ya wasiwasi uliooneshwa na Ujerumani na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya.
Soma pia:Jeshi la Israel lawaua 'magaidi tisa' wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi
Hakutarajiwi kufanyika maamuzi yoyote rasmi kwenye mkutano huu usio rasmi, ambao ulitarajiwa kufanyika Budapest, Hungary, lakini badala yake ulihamishiwa Brussels, kama njia ya kumsusia Rais Viktor Orban kutokana na mkutano wake na Rais Vladimir Putin wa Urusi.