1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yawaua Wapalestina tisa katika Ukingo wa Magharibi

28 Agosti 2024

Israel imesema ´magaidi´ tisa wa Kipalestina wameuawa wakati wa oparesheni iliyofanyika katika Ukingo wa Magharibi. Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limesema operesheni hiyo kubwa inaweza kuendelea kwa siku kadhaa.

https://p.dw.com/p/4k0FO
Wapalestina wakitafkari gari iliyoharibiwa wakati wa operesheni ya jeshi la Isreal
Wapalestina wakitafkari gari iliyoharibiwa wakati wa operesheni ya jeshi la IsrealPicha: Ali Sawafta/REUTERS

Israel imesema ´magaidi´ tisa wa Kipalestina wameuawa wakati wa oparesheni iliyofanyika katika Ukingo wa Magharibi.Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limesema operesheni hiyo kubwa inaweza kuendelea kwa siku kadhaa.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema wanaume wawili waliuawa katika mji wa Jenin na saba mjini Tuba mapema leo. Wizara hiyo imewatambua wawili waliouawa mjini Jenin kuwa Qassam Muhammad Jabarin mwenye umri wa miaka 25, na Asema Walid Balout mwenye umri wa miaka 39.

Soma: Jeshi la Israel lamkombowa mateka mmoja kusini mwa Gaza

Wakati huo huo, wizara ya afya kwenye Ukanda wa Gaza imesema mpaka sasa Wapalestina zaidi ya elfu 40 wameshauawa katika vita hivyo kati ya Israel na wapiganaji wa kipalestina vilivyoanza miezi 11 iliyopita. Idadi hiyo inajumuisha Wapalestina wapatao 58 waliouawa mnamo muda wa saa 24 zilizopita. Kwa mujibu wa wizara hiyo, Wapalestina wengine wapatao 93,778 wamejeruhiwa.