1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi la Israel lamkombowa mateka mmoja kusini mwa Gaza

27 Agosti 2024

Vikosi maalum nchini Israel vimemkomboa mateka mmoja wa nchi hiyo aliyekuwa miongoni mwa waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo la Hamas katika uvamizi wa Oktoba 7.

https://p.dw.com/p/4jycN
Vikosi vya Israel
Vikosi vya Israel Picha: NICOLAS GARCIA/AFP/Getty Images

Vikosi maalum nchini Israel vimemkomboa mateka mmojawa nchi hiyo aliyekuwa miongoni mwa waliotekwa nyara na kundi la wanamgambo la Hamas katika uvamizi wa Oktoba 7.

Soma: Mashambulizi ya anga ya Israel yawaua watu 18 Gaza

Mateka huyo alikombolewa katika njia za chini kwa chini Kusini mwa Ukanda wa Gaza kufuatia operesheni ngumu. Mateka huyo ametambuliwa kama Qaida Farhan Alkadi mwenye umri wa miaka 52 kutoka jamii ya mabedui  ya Kusini mwa Israel.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amefahamisha kwamba Alkadi amekombolewa kutoka njia za chini kwa chini za Gaza lakini hakutowa ufafanuzi zaidi kuhusu operesheni hiyo kutokana na kile alichosema ni sababu za kiusalama zinazohusu  mateka wengine waliobakia.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW