Wakati ulimwengu ukihimiza matumizi ya nishati ya kijani, kijana Frednand Laulian ametumia maarifa yake kutengeneza pikipiki isiyotumia mafuta akiwa na lengo la ulinzi wa mazingira lakini kukabiliana na kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta kusikotabirika.