1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karua Kumtetea Besigye kwenye mahakama ya kijeshi Uganda

6 Januari 2025

Baraza la wanasheria nchini Uganda hatimaye limetoa leseni ya muda kwa mwanasheria na mwanasiasa wa Kenya Martha Karua, kumtetea mwanasiasa wa upinzani Dokta Kizza Besigye katika mahakama ya jeshi.

https://p.dw.com/p/4os68
Uganda Kizza Besigye Oppositionspolitiker
Mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye akionyesha alipowasili katika Mahakama ya Kijeshi ya Makindye mjini Kampala, Novemba 20, 2024.Picha: BADRU KATUMBA/AFP

Hatua hii ni baada ya mashirikisho ya Kenya na Afrika Mashariki kuwasilisha malalamiko katika mahakama ya Jumuiya Ya Afrika Mashariki. Mwezi Desemba mwaka jana, baraza hilo lilikataa kumpa leseni Martha Karua kwa msingi kwamba uhusika wake katika kesi hiyo ulikuwa na hila za kisiasa na kwamba asingekuwa na umuhimu mkubwa kwa sababu Dkt Besigye anao mawakili wengine. Pamoja na hayo, Dkt Besigye alishikilia kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kukataa maamuzi yake ya kumfanya Martha Karua kuwa kiongozi wa jopo la mawakili wake 40. Hii ndiyo ilisababisha mkwamo kesi dhidi yake kuendelea na kuahirishwa mwa muda wa wiki mbili hadi hapo kesho tarehe saba mwezi Januari mwaka huu. Dokta Besigyena mwenzake Sheikn Obed Lutale wamebaki gerezani tangu walipofikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya kufanya njama za kuvuruga usalama wa Uganda pamoja na makosa ya kupatikana na bastola mbili katika hoteli moja mjini Nairobi. Wawili hao walikamatwa katika mazingira ambayo yametajwa kuwa ya utekaji nyara na kusafirishwa hadi Kampala.