SiasaUswisi
Makubaliano ya NATO ya Uswidi yanaweza kufikiwa
5 Juni 2023Matangazo
Stoltenberg ameyasema hayo baada ya kukutana mjini Istanbul na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye ataendeleza muhula wake wa uongozi kwa miongo miwili baada ya kushinda uchaguzi.
Soma pia:NATO yajadili hakikisho la usalama wa Ukraine baada ya vita
Katibu mkuu huyo wa NATO amesema pia kuwa maafisa kutoka Uturuki, Sweden na Finland watakutana kwa mazungumzo baadaye mwezi huu ili kujaribu kuondoa pingamizi kutoka kwa Uturuki na Hungary ambazo zimeichelewesha Sweden kujiunga na NATO.