NATO yajadili hakikisho la usalama wa Ukraine baada ya vita
1 Juni 2023Matangazo
Hata hivyo, zikisalia wiki takriban tano tu hadi kufanyika kwa mkutano wa kilele wa NATO, nchi wanachama wa jumuiya hiyo zina maoni yanayokinzana juu ya ombi la Ukraine kujiunga na NATO.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, akisaidiwa na nchi za Ulaya mashariki, anataka mkutano wa kilele wa Julai upeleke ujumbe mzito kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa NATO baada ya vita vya Urusi kumalizika.
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema nchi zote wanachama zinakubaliana na ahadi ya mwaka 2018, kuwa siku moja Ukraine itakuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ya kujihami.
Hata hivyo, wanadiplomasia wanasema Marekani yenye ushawishi mkubwa ndani ya NATO, haitaki kwenda mbali zaidi na ahadi hiyo yenye utata.