Erdogan aapishwa tena kuwa rais wa Uturuki kwa miaka mitano
3 Juni 2023Matangazo
Wakati wa kiapo chake Erdogan amesema atakubali maoni ya wananchi na kuheshimu haki za binaadamu. Upande wa upinzani haukusimama wakati rais huyo wa Uturuki alipokuwa anakula kiapo cha kuchukua tena madaraka.
Erdogan ashinda duru ya pili ya uchaguzi Uturuki
Erdogan, anayeingia kwenye muhula wa tatu madarakani, anatarajiwa kulitangaza baraza lake la mawaziri baada ya sherehe za uapisho. Katika uchaguzi wa wiki iliyopita uliomuweka madarakani, Rais huyo wa Uturuki aliungwa mkono kwa asilimia 52.
Sherehe za uapisho zitafuatiwa na hafla itakayofanyika katika kasri la Rais na inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi kutoka mataifa 78, na mashirika ya kimataifa.