1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMarekani

Maelfu watakiwa kuhama baada ya moto mpya kuzuka Marekani

23 Januari 2025

Maelfu ya wakazi kusini mwa mji wa California wametakiwa kuondoka baada ya kuzuka moto mpya wa nyikani, kaskazini mwa Los Angeles, na kusambaa takriban kilomita za mraba 41 katika muda mfupi.

https://p.dw.com/p/4pVQY
USA Castaic 2025 | Hughes-Feuer in Los Angeles County
Wazima moto wakipambana kuudhibiti moto uliopewa jina "Hughes Fire" kaskazini mwa Los Angeles.Picha: Mario Tama/Getty Images

Moto huo uliopewa jina la Hughes Fire, unawaka karibu na eneo maarufu la burudani karibu na Ziwa Castaic, kama kilomita 64 kutoka eneo kulikowaka moto mkubwa kabisa, ambao bado haujazimwa kikamilifu tangu ulipozuka Januari 7.

Soma pia: Waliofariki katika moto wa nyika Los Angeles wafikia 16

Mkuu wa polisi katika kaunti ya Los Angeles Robert Luna amesema zaidi ya watu 31,000 wameagizwa kuondoka hadi sasa.

Amesema, "Na hivi sasa, idadi niliyonayo ni kwamba kuna takriban watu 31,000 ambao watatakiwa kuhama. Wengine 23,000 pia wataathirika kufuatia maonyo haya ya kuhama."

Bado haijajulikana ikiwa kuna mali zilizoharibiwa na moto huo mpya.