SiasaUfaransa
Macron aahidi kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa, Niger
25 Septemba 2023Matangazo
Tangazo hilo, ni pigo kubwa dhidi ya sera za Ufaransa barani Afrika, baada ya wanajeshi wa taifa hilo pia kuondoka taifa jirani la Mali na Burkina Faso katika miaka ya karibuni baada ya kukumbwa na mapinduzi.
Ufaransa iliwabakiza wanajeshi wake 1,500 nchini Niger tangu mapinduzi ya Julai na mara kadhaa imekaidi agizo la utawala mpya wa kijeshi la kumuondoa balozi wake, kwa kuwa Ufaransa haiutambui utawala huo.
Mapinduzi ya kijeshi nchini Niger yalimuondoa madarakani rais Mohamed Bazoum.
Taifa hilo lilipeleka maelfu ya wanajeshi kwenye ukanda wa Sahel baada ya wakuu wa mataifa hayo kuiomba kusaidia harakati zao za kupambana na ugaidi.