1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yampa balozi Sylvain Itte, saa 48 kuondoka nchini humo

26 Agosti 2023

Watawala wa kijeshi wa Niger walioingia madarakani baada ya kuipindua serikali mwezi Julai, wamempa balozi wa Ufaransa Sylvain Itte, saa 48 kuondoka nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Vbel
Niger Französische Botschaft in Niamey
Picha: AFP

Agizo hilo limetolewa kupitia wizara ya mambo ya kigeni ya nchi hiyo. 

Kufuatia hatua hiyo, Ufaransa imejibu kwa kuipinga amri hiyo iliyotolewa dhidi ya balozi wake na kusema kwa mara nyinine kuwa, haitambui mamlaka ya utawala huo wa kijeshi. 

Burkina Faso na Mali zatangaza vita dhidi ya yeyote atakaeivamia Niger

Uhusiano baina ya Niger na baadhi ya mataifa ya magharibi, umedorora tangu yalipotokea mapinduzi nchini humo Julai 26. 

Amri ya kumtaka balozi wa Ufaransa aondoke Niger, imetolewa siku kadhaa baada ya Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika ya Magharibi ECOWAS, kutishia kuchukua hatua za kijeshi ili kubatilisha mapinduzi ya mwezi uliopita, yaliyomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum.