1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Maafisa wa Italia washtakiwa baada ya vifo vya wahamiaji

23 Julai 2024

Italia imefungua mashtaka dhidi ya maafisa sita kwa kuwahusisha na vifo vya wakimbizi, ikiwa ni miezi 18 baada ya boti yao kuzama katika bahari ya Mediterania, ambapo inadhaniwa ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

https://p.dw.com/p/4idiv
Italia
Maafisa sita wa Italia washtakiwa baada ya vifo vya wahamiajiPicha: Johan Ben Azzouz/Photopqr/Voix du Nord/MAXPPP/dpa/picture alliance

Mamlaka ya mahakama ya taifa hilo leo hii imearifu kuwa maafisa wa  mpango wa ulinzi wa pwani na polisi wa forodha lazima wapande kizimbani kwa kushindwa kutoa msaada.

Mtuhumiwa mmoja ambae anahusisha na usafirishaji haramu wa watu amehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kukutwa na hatia ya janga hilo. Washukiwa wengine watatu wa biashara hiyo ya magendo pia wanatazamiwa kukabiliwa na kesi.

Umoja wa Mataifa wasema wahamiaji na wakimbizi zaidi kutoka Afrika wanaelekea Kaskazini kupia Mediterania

Februari mwaka jana, boti iliyokuwa imetokea pwani ya Uturuki, ikiwa imewapakia zaidi ya watu 150, ilikuwa katika jaribio la kuwavusha wahamiaji kupitia bahari ya Mediterania, hadi kusini mwa Italia.