UN: Wahamiaji zaidi wakimbilia Ulaya kupitia Mediterania
5 Julai 2024Umoja wa mataifa na washirika wake wamesema wahamiaji na wakimbizi zaidi kutoka barani Afrika wanaelekea maeneo ya Kaskazini kuelekea bahari ya Mediterranea na Ulaya wakipitia njia hatari katika eneo la jangwa la Sahara.
Wamesema eneo hilo pia kunapatikana magenge ya uhalifu yanayoendesha matukio ya utumwa, kuwanyofowa viungo vyao vya mwili, ubakaji, kuwafanyia matukio mengine ya unyanyasaji pamoja na kuwateka nyara, wakidai kikombozi.
Ripoti iliyochapishwa Ijumaa hii na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kushughulikia wakimbizi na wahamiaji imekadiria kwamba njia za ardhini zinazotumiwa na wakimbizi na wahamiaji barani Afrika kuelekea Ulaya ni hatari kama zilivyo njia za kupitia bahari ya Mediterrania.
Ripoti hiyo imesema vita vipya pamoja na ukosefu wa uthabiti katika mataifa kama Mali,BurkinaFaso na Sudan yamechangia ongezeko la idadi ya wakimbizi wanaofanya safari kuelekea bahari ya Mediterrania.