1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yatishia kuishambulia Ulaya

14 Julai 2024

Ikulu ya Kremlin imetahadharisha kuwa, ikiwa Marekani itapeleka makombora ya masafa marefu nchini Ujerumani, miji mikuu ya mataifa ya Ulaya huenda ikalengwa na makombora ya Urusi

https://p.dw.com/p/4iGgs
Kombora la masafa marefu Tomahawk
Toleo jipya la makombora masafa marefu aina ya TomahawkPicha: Everett Collection/picture alliance

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, ameyasema hayo kupitia televisheni ya taifa ya Russia 1, siku chache baada ya Washington kutangaza wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO,kuwa itapeleka silaha hizo Ujerumani kuanzia mwaka 2026 yakiwemo makombora aina ya Tomahawk.

Soma zaidi: Urusi: Kupeleka silaha Ujerumani kutachochea Vita Baridi kama ilivyotokea huko nyuma

Kremlin imeikosoa hatua hiyo na kusema Marekani inaelekea kuanzisha tena vita baridi na kwamba kufanya hivyo kunaashiria kuwa taifa hilo linashiriki moja kwa moja kwenye mzozo wa Ukraine. Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ameupongeza uamuzi wa Marekani licha ya kukosolewa na wanachama wa chama chake cha SPD.