Korea Kusini yahairisha kutuma satelaiti ya kijasusi
28 Novemba 2023Korea Kusini imeahirisha mipango yake ya kutuma satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi katika mzingo wa dunia, siku chache tu baada ya hasimu wake Korea Kaskazini kurusha satelaiti yake ya kijasusi kwa mara ya kwanza.
Chini ya mkataba wa SpaceX, Korea Kusini ilitarajiwa kutuma satelaiti tano za kijasusi katika mzingo wa dunia kufikia mwaka 2025 na urushaji wake wa kwanza ulikuwa umepangwa kufanyika katika kambi ya jeshi la anga la Marekani ya Vandenberg mjini California.
Soma pia:Korea Kusini yasitisha mkataba wa kijeshi na Korea Kaskazini
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema katika taarifa yake kuwa, urushaji wa satelaiti ulichelewa kutokana na hali mbaya ya hewa. Maafisa wa wizara wameongeza kuwa, urushaji huo umepangwa kufanyika tena Jumamosi ijayo.