Pyongyang yadai kunasa picha za satelaiti yake ya kijasusi
25 Novemba 2023Satelaiti hiyo imegundua sehemu mbalimbali za kimkakati kama kambi za jeshi la Marekani na maeneo kadhaa huko Korea Kusini. Lakini Seoul imesema ni mapema mno kubaini ikiwa satelaiti hiyo inafanya kazi kama anavyodai jirani yake Pyongyang.
Hata hivyo, wanadiplomasia wakuu wa Marekani, Korea Kusini na Japan wamefanya mazungumzo ya simu kulijadili tukio hilo ambalo pia wameliGuterres alaani hatua ya Korea Kaskazini ya kurusha satelaiti ya kijasusi katika mzingo wa dunialaani vikali.
Soma pia:Guterres alaani hatua ya Korea Kaskazini ya kurusha satelaiti ya kijasusi katika mzingo wa dunia
Wataalamu wanasema kitendo cha Korea Kaskazini kurusha satelaiti ya upelelezi inayofanya kazi, kutaboresha uwezo wa taifa hilo wa kukusanya taarifa za kijasusi hasa kumhusu jirani yake Korea Kusini, na kutoa taarifa muhimu katika mzozo wowote wa kijeshi.