1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres ailaani Korea Kaskazini kwa kurusha satelaiti

22 Novemba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelani hatua ya Korea Kaskazini ya kurusha setilaiti ya upelelezi katika mzingo wa dunia.

https://p.dw.com/p/4ZHun
Urushwaji setilaiti ya upelelezi ya Korea Kaskazini
Urushwaji setilaiti ya upelelezi ya Korea Kaskazini katika mzingo wa duniaPicha: KCNA/AP/picture alliance

Msemaji wa Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq, ameeleza kuwa Guterres amelaani vikali kurushwa kwa satelaiti ya kijeshi ya Korea Kaskazini kwa kutumia teknolojia ya makombora ya balistiki.

Haq ameongeza kuwa, urushwaji wa setilaiti hiyo ya kijasusi katika mzingo wa dunia unakwenda kinyume na maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Hilo ni jaribio la tatu la Korea Kaskazini la kurusha satelaiti katika mzingo wa dunia, baada ya majaribio mawili ya awali kufeli.