1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini imepanga kurusha satelaiti kesho.

21 Novemba 2023

Korea Kaskazini imetoa taarifa kwa Japan kuhusu nia yake ya kurusha satelaiti hapo kesho.

https://p.dw.com/p/4ZFaP

Hayo ni kulingana na taarifa ya mamlaka za Tokyo na  hatua hiyo itakuwa inakaidi maonyo ya Seoul na kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayopiga marufuku Pyongyang kutumia teknolojia ya makombora ya masafa marefu. Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ameonya kuhusu hatua hiyo na kusema Japan, Korea Kusini na Marekani wanaratibu majibu. Jaribio hili jipya la Korea Kaskazini, ambalo linaweza kufanyika kati ya Novemba 22 na Desemba 1 kwa mujibu kituo cha walinzi wa pwani wa Japan, litakuwa la tatu kwa Korea Kaskazini, baada ya kushindwa mara mbili kurusha satelaiti ya kijeshi angani mnamo mwezi Mei na Agosti mwaka jana. Korea Kusini imeonya kuwa mara hii Pyongyang huenda ikafanikisha azma hiyo baada ya kupokea ushauri wa kiufundi kutoka kwa Urusi.