1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yajiandaa na majaribio ya makombora

17 Agosti 2023

Korea Kaskazini inaandaa jaribio lake la pili la kuweka satelaiti ya kijasusi angani pamoja na majaribio ya makombora ya masafa marefu kuadhimisha kumbukumbu muhimu ya kitaifa.

https://p.dw.com/p/4VI0k
Nordkorea Treffen der Zentralen Militärkommission der Arbeiterpartei Koreas in Pjöngjang
Picha: KCNA/REUTERS

Korea Kaskazini inaandaa jaribio lake la pili la kuweka satelaiti ya kijasusi angani pamoja na majaribio ya makombora ya masafa marefu kuadhimisha kumbukumbu muhimu ya kitaifa.

Majaribio hayo yanafanyika piakupinga mipango ya Marekani ya kuimarisha mifungamano ya kikanda. Shirika la ujasusi la Korea Kusini limetoa taarifa hiyo kwa wabunge wa nchi hiyo.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un alitarajiwa kufanya majaribio ya silaha kujibu mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini.

Soma pia:Japan,Marekani kuunda mfumo kisasa kuzuia makombora masafa marefu

Shirika la upelelezi la Korea Kusini limesema majaribio ya silaha ya Korea Kaskazini pia ni ishara ya kupinga mkutano wa kilele wa viongozi wa Marekani, Japan na Korea Kusini.

Shirika hilo limewaambia wabunge wa nchi hiyo huenda Korea Kaskazini ikajaribu tena kupeleka satelaiti ya kijasusi anganimwisho wa mwezi huu. Jaribio la kwanza la kurusha satelaiti hiyo lilishindikana mnamo mwezi Mei. Satelaiti hiyo ya kwanza iliangukia baharini.

Korea Kaskazini yafyatua tena makombora