1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Kenya yatuma wanajeshi zaidi nchini Haiti

19 Januari 2025

Kenya imetuma maafisa 217 zaidi wa polisi nchini Haiti, kama sehemu ya jeshi la kimataifa la kukabiliana na ghasia za magenge katika taifa hilo la Karibia.

https://p.dw.com/p/4pL46
Polisi wa Kenya-Haiti
Polisi wa Kenya wakishika doria katika mji mkuu unaotishwa na magenge nchini Haiti.Picha: DW

Kulingana na waziri wa mambo ya ndani, Kipchumba Murkomen, maafisa hao waliondoka Kenya siku ya Ijumaa. Murkomen ameongeza kuwa misheni hiyo inayoongozwa na Kenya imepiga hatua kubwa katika kupunguza vurugu za magenge, na kupata sifa kote ulimwenguni, na kwamba ahadi ya kujitolea kwa taifa hilo la Afrika Mashariki haiyumbishwi.

Kenya ilituma wanajeshi wake Haiti kwa mara ya kwanza mwezi Juni na kufikia sasa imetuma zaidi ya wanajeshi 600. Rais William Ruto aliahidi kupeleka wanajeshi 1,000 kama sehemu ya kikosi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Haiti.

Soma pia: Magenge ya Haiti yaendeleza ghasia nje ya mji mkuu

Vurugu za magenge zimeacha zaidi ya Wahaiti 700,000 bila makao huku wengi wakisongamana katika makazi ya muda na yasiyo safi

baada ya nyumba zao kubomolewa. Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 5,600 waliripotiwa kuuawa kote Haitimwaka jana.