SiasaHaiti
Magenge ya Haiti yaendeleza ghasia nje ya mji mkuu
23 Oktoba 2024Matangazo
Maria Isabel Salvador ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa magenge yametanua operesheni zao nje ya mji mkuu Port-au-Prince, na hata kuzishambulia boti ndogo na kuwateka nyara maafisawa kampuni za usafirishaji wa mizigo. Bi Salvador amesema hali nchini humo imeendelea kuwa mbaya katika miezi mitatu iliyopita, huku zaidi ya watu 700,000 sasa wakiwa wamepoteza makaazi. Aidha ameongeza kuwa mchakato wa kisiasa nchini humo unakabiliwa na changamoto kubwa. Kauli ya Bi Salvador imetolewa wiki chache tu baada ya raia 115 kuuawa na makumi ya wengine wakijeruhiwa katika shambulio la wahalifu katika mji wa kati wa Port Sonde, tukio ambalo amesema liligubikwa na ukatili wa kupindukia.