Kampeni za uchaguzi mkuu zaanza rasmi Kongo
20 Novemba 2023Takriban wagombea 25 wanawania kiti hicho cha urais wakati kukiwa na joto kali la kisiasa na mapigano pia yakishuhudiwa Mashariki kwa taifa hilo.
Watu milioni 44 kati ya milioni 100 ya Idadi Jumla ya watu nchini humo wamesajiliwa kushiriki uchaguzi huo uliopangiwa kufanyika tarehe 20 Desemba.
Soma pia:Kongo: Kipenga cha kampeni za uchaguzi chapulizwa
Katika uchaguzi huo, wapiga kura pia watawachagua wabunge, madiwani na viongozi wa serikali za mitaa katika nchi hiyo iliyo na rasilimali kubwa lakini inayokumbwa na migogoro ya mara kwa mara pamoja na ufisadi.
Miongoni mwa wapinzani wa kuu wa Tshisekedianaetetea kiti chake ni pamoja na mshindi wa amani ya Nobel Denis Mukwege, gavana wa zamani wa mkoa wa utajiri wa madini wa Katanga Moise Katumbi, na aliyemaliza wa pili katika uchaguzi wa rais mwaka wa 2018 Martin Fayulu.