1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za uchaguzi DRC kuanza rasmi Jumatatu

19 Novemba 2023

Kampeni za uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinaanza rasmi kesho Jumatatu na zitaendelea kwa muda wa mwezi mmoja.

https://p.dw.com/p/4Z91t
Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo | Mfuasi wa Felix Tshisekedi
MMoja ya wafuasi wa Rais Felix Tshisekedi Tshilombo aliyewasilisha ombi la kuwania tena kiti hicho, katika mji wa Kinshasa, Oktoba 7, 2023.Picha: Justin Makangara/REUTERS

Wagombea 26 wanatarajiwa kuwania urais huku kukiwa na wasiwasi wa hali ya kisiasa na mapigano mashariki mwa nchi hiyo.

Kampeni za awali zimekuwa zikiendelea kwa muda, huku Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili, akihudhuria hafla nyingi za umma na washirika wake wakijivunia rekodi yake.

Kwenye siku ya ufunguzi, Tshisekedi atafanya mkutano katika uwanja wa Mashahidi, mjini Kinshasa huku mmoja wa wapinzani wake wakuu, Martin Fayulu, akihutubia mkutano katika mkoa jirani na Kishansa.

Takriban wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha, kati ya wakazi karibu milioni 100, watamchagua rais mnamo, Disemba 20, pamoja na maelfu ya wagombeaji wa ubunge na serikali za mitaa katika taifa hilo.