Jeshi la Myanmar kuwaruhusu raia 'watiifu' kubeba silaha
14 Februari 2023Watu hao wanapaswa kutii maagizo kutoka kwa serikali za mitaa kushiriki hatua za utekelezaji wa sheria na usimamizi wa usalama.
Tangazo hilo limechochea hofu ya kutokea ghasia zaidi katika nchihiyo iliyoharibiwa na kile ambacho baadhi ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekiita vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Soma pia:Myanmar yatangaza hatua mpya kali dhidi ya 'habari za uongo'
Waraka wa kurasa 15 kuhusu sera mpya ya silaha unaohusishwa na wizara ya mambo ya ndani ulisambazwa awali kupitia akaunti za mtandao wa Facebook zinazounga mkono jeshi.
Jeshi liliipinduwa serikali iliyochaguliwakidemokrasia ya Aung San Suu Kyi miaka miwili iliyopita, na kusababisha maandamano ya amani yaliyoenea, ambayo yaligeuka kuwa upinzani wa silaha baada ya vikosi vya usalama kutumia nguvu kubwa kukandamiza upinzani wote.