SiasaMyanmar
Jeshi la Myanmar latuhumiwa kwa uhalifu wa kivita Ujerumani
24 Januari 2023Matangazo
Kesi hiyo iliwasilishwa kwa Mwendesha mashitaka mkuu wa Ujerumanichini ya kanuni ya kufunguliwa kesi popote pale ulimwenguni, ambayo inaruhusu kuendeshwa kwa kesi za makosa kadhaa makubwa ya uhalifu bila kujali yalikofanyika, na imetumika kuwashitaki Wasyria kuhusiana na uhalifu uliofanywa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Walalamikaji hao 16 wanaishi katika nchi tofauti, ikiwemo Myanmarna wanatoka kwenye makabila mbalimbali ya nchi hiyo, ikiwemo jamii ya Rohingya, Burman ambayo ndio walio wengi, na China ya walio wachache.
Malalamiko yao yanaanzia mwaka wa 2017, wakati nchi hiyo ilikuwa chini ya utawala wa kiraia hadi mwaka wa 2021, baada ya mapinduzi yaliyoliweka jeshi madarakani.