IGAD ina matumaini ya mazungumzo kati ya ethiopia na OLA
22 Novemba 2023Duru ya pili ya mazungumzo ya amani kati ya Addis Ababa na OLA, yalishindwa kuleta matokeo licha ya uungwaji mkono wa IGAD na washirika wa kimataifa.
Pande zote mbili zilishtumiana kwa kuzuwia maendeleo kwenye mazungumzohayo yaliofanyika nchini Tanzania, yakiwa na lengo la kumaliza uasi wa miaka mitano uliohusisha mauaji ya kikabila ya raia.
Soma pia:Jeshi la Ethiopia larejesha udhibiti mji wa Lalibela
Katibu Mtendaji wa IGAD, Worknen Gebeyehu ametoa wito kwa pande zote kuzingatia dhamira yao kwa mchakato wa amani kwa maslahi bora ya watu wa Ethiopia.
Kundi la OLA ambalo limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na serikali ya Addis Ababa, limekuwa likipigana dhidi ya serikali tangu 2018, baada ya kujitenga na chama cha Ukombozi wa Oromo, OLF, kilipotangaza kuachana na mapambano ya silaha.