HRW: Yataka Ethiopia iwekewe shinikizo ili haki ipatikane
2 Novemba 2023Matangazo
Shirika hilo la haki za binadamu linasema vikosi vya Eritrea vilivyoungwa mkono na serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, vilifanya mauaji, udhalilishaji wa kingono, utekaji wa watu, kuzuia kazi ya usambazaji wa misaada ya kiutu na kazi ya mashirika ya uangalizi ya Umoja wa Afrika, kufuatia kutiwa saini mkataba wa amani.
Licha ya mwaka mmoja wa mkataba wa amani, mapigano yanaendelea Ethiopia
Mkataba wa amani, uliosimamiwa na Afrika Kusini na Umoja wa Afrika mnamo Novemba 2 mwaka jana, ulifikisha mwisho mapigano ya Tigray ila kutokea wakati huo, kumeibuka machafuko katika sehemu nyingine za nchi hiyo hasa katika jimbo la Amhara.
Vikosi kutoka Amhara vliliunga mkono jeshi la serikali wakati wa vita hivyo.