1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris na Walz watetea sera zao mbele ya Wamarekani

30 Agosti 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris jana Alhamisi ameitetea misimamo yake ya kisera wakati wa mahojiano ya kwanza ya televisheni tangu aanze kampeni zake za urais.

https://p.dw.com/p/4k6YU
Marekani | Kamala Harris na Tim Walz.
Mgombea urais Marekani wa chama cha Demokrati Kamala Harris na mgombea mwenza Tim Walz.Picha: Anna Moneymaker/Getty Images

Harris aliyekuwa na mgombea mwenza wake, Gavana wa Minnnesota Tim Walz, alizungumzia masuala mapana kuanzia uhamiaji haramu, uchumi hadi mzozo katika Ukanda wa Gaza, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN:

"Joe Biden na mimi na serikali yetu tulishirikiana na Bunge kuhusu suala la uhamiaji ambalo ni muhimu sana kwa watu na usalama wetu, ambalo ni mpaka. Na kutokana na kazi hiyo, ulitungwa muswada ambao tuliuunga mkono na Donald Trump alitaarifiwa kuhusu muswada huu ambao ungechangia kulinda mpaka wetu.  Alisema Kamala.

Soma pia:Harris na Walz wameanza msafara wa basi wa kampeni katika jimbo la Georgia
  
Harris pia ameahidi kumteua mjumbe kutoka kwenye chama cha Republican kuhudumu kwenye baraza lake la mawaziri ikiwa atachaguliwa.

Harris aidha amepuuzilia mbali hoja za mpinzani wake, Donald Trump, kuhusiana na utambulisho wake, na kumwambia Wamarekani wako tayari kufungua ukurasa mpya dhidi ya mgawanyiko uliosababishwa na mgombea huyo wa Republican.