1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris na Walz waanza kampeni katika jimbo la Georgia

28 Agosti 2024

Mgombea urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Kamala Harris na mgombea mwenza Tim Walz, wataanza msafara wa basi kuendesha kampeni ya pamoja kwenye jimbo la Georgia.

https://p.dw.com/p/4k1OR
Kamala Harris na mgombea mwenza Tim Walz
Kamala Harris na mgombea mwenza Tim WalzPicha: Joe Lamberti/AP/dpa/picture alliance

Mgombea urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Kamala Harris na mgombea mwenza Tim Walz, wataanza msafara wa basi kuendesha kampeni ya pamoja kwenye jimbo la Georgia, ambapo chama hicho kilipata ushindi finyu katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Soma kuhusu: Kamala akubali rasmi uteuzi wa kugombea urais Marekani

Katika uchaguzi wa safari hii jimbo hilo linaweza kuwa na dhima kubwa. Kasi ya uchaguzi imebadilika tangu Harris alipopitishwa na chama chake kuwa mgombea na anayo matumaini ya kuzivutia kura za Wamerakani weusi ambao kwa pamoja ni thuluthi ya wapiga kura kwenye jimbo la Georgia watakaokuwa muhimu katika kumwezesha bibi, Harris kupata ushindi.

Wakati huo huo, mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump, na mpinzani wake wa chama cha Democratic Harris watapambana mwezi ujao katika mdahalo wa kwanza wa urais. Itakuwa nafasi ya kwanza kwa wapiga kura wapatao milioni 240 wa Marekani kupata kuwasikia Trump na Harris wakieleza sera zao bega kwa bega, na kwenye ukumbi mmoja.