Guterres alalamikia mataifa kutumia pesa katika silaha
14 Februari 2024Matangazo
Guterres ameyasema hayo katika mkutano wa Baraza la Usalama uliyohusu kuhusu uhusiano kati ya chakula, mabadiliko ya tabia nchi na migogoro. Amesema inasikitisha kuona serikali zikitumia gharama kubwa kununua silaha, huku zikikabiliwa na njaa katika bajeti ya uhakika wa chakula, mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu zaidi.Katibu mkuu huo wa Umoja wa Mataifa alionya kwa kusema bila ya kuchukuliwa hatua hali itazidikuzorotahuku Beth Bechdol, naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, akitoa mfano wa nchi kama Burkina Faso, Mali na Niger.