1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yaipa Kenya masharti ya mazungumzo baina yao

7 Agosti 2023

Ethiopia imetoa masharti makali kwa serikali ya Kenya kabla ya kushiriki mazungumzo ya amani ya kutuliza wasiwasi katika eneo la mpaka baina ya nchi hizo mbili baada ya kutokea mauaji ya raia wa Ethiopia wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4Ur5d
Kenia Dürre an der Grenze zu Äthiopien
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Miongoni mwa masharti hayo, ni pamoja na kurejeshwa kwa mifugo yote iliyoibwa kutoka kwa raia hao waliouwawa.

Ujumbe wa Ethiopia ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dilo, Goraye Galgalo Jaldesa, umesema jamii ya Ethiopia bado ina hasira na hivyo kuna haja kwa serikali ya Kenya kutuliza joto kwa kurejesha mifugo yote iliyoporwa.

Soma: Mazunguzo ya amani ya Kenya na Ethiopia yaendelea

Wakati huo huo, serikali ya Kenya imetoa muda wa siku saba kwa jamii inayoishi mpakani kusalimisha mifugo hiyo au viongozi wote wa eneo hilo watasimamishwa kazi. 

Kamishna wa Marsabit aliyeongoza ujumbe wa Kenya katika mashauriano ya awali na Ethiopia, Norbert Komora, amesema iwapo mifugo yote itarejeshwa, hali ya utulivu itarejea kwenye eneo la mpaka.