1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS wakubaliana uwezekano wa kuingilia kati kijeshi Niger

5 Agosti 2023

Wakuu wa majeshi kutoka nchi za Jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi ya ECOWAS wamekubaliana juu ya uwezekano wa mpango wa kuingilia kati kijeshi nchini Niger.

https://p.dw.com/p/4Unzk
Mkutano wa ECOWAS kuhusu mzozo wa Niger
Mkutano wa ECOWAS kuhusu mzozo wa NigerPicha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Ni baada ya viongozi wa mapinduzi kushindwa kurejesha utawala wa kiraia. Wakuu hao walikutana mjini Abuja Nigeria, kujadili njia za kushughulikia mgogoro huo, ambao ni wa hivi karibuni katika mkururo wa mapinduzi ya kijeshi katika eneo la Sahel tangu mwaka 2020.

Soma zaidi: Viongozi wa kijeshi wa Niger kujibu jaribio lolote la kichokozi

Kamishna wa ECOWAS Abdel-Fatau Musah amesema vipengele vyote vya uwezekano wa uingiliaji kati kijeshi vimefanyiwa kazi. Vipengele hivyo vinajumuisha rasilimali zinazohitajika na lini wanaweza kutuma wanajeshi.

Viongozi wa mapinduzi wa Niger wameonya kwamba jaribio lolote la kuingilia kati nchi hiyo litakabiliwa na upinzani na kuungwa mkono na nchi jirani za Mali na Burkina Faso zilisema hatua hizo zitakuwa ni tangazo la vita.