1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken aanza ziara ya siku tano barani Afrika

21 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Anthony Blinken ameanza ziara yake Barani Afrika, kujadili ushirikiano wa Marekani na Afrika katika masuala ya biashara, mabadiliko ya tabia nchi, miundombinu na afya.

https://p.dw.com/p/4bVcx
USA/Blinken
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Anthony Blinken Picha: Evelyn Hockstein/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Kulingana na wizara yake, Blinken ataanzia ziara yake Cape Verde, Ivory Coast, Nigeria na Angola kuanzia Januari 21 hadi Januari 26.

Changamoto za usalama katika mataifa ya Afrika Magharibi kufuatia mapinduzi yaliyofanyika Niger mwaka uliopita ni mambo muhimu yatakayojadiliwa katika ziara ya Blinken barani Afrika.

Blinken kuzuru Afrika wakati mizozo ikiendelea kutatiza sera ya kigeni ya Marekani

Msaidizi wa Blinken anayeshughulikia masuala ya Afrika, Molly Phee amesema Marekani ina rekodi inayojulikana na anatumai jeshi lililochukua madaraka nchini Niger litaichagua Marekani kuliko kuwa mshirika na Urusi.