1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua kubwa zavuruga usafirishaji mizigo, bandari ya Mombasa

19 Novemba 2023

Kampuni ya reli inayomilikiwa na serikali ya Kenya imesema huduma za mizigo ya kwenda na kurudi katika mji wa bandari wa Mombasa zimekatizwa kwa sababu ya mvua kubwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la pwani.

https://p.dw.com/p/4Z927
Mafuriko nchini Kenya
Picha ikionyesha mafuriko ya maji karibu na daraja la Sigiri, baada ya Ziwa Nzoia kupasuka kufuatia mvua kubwa. Hii ilikuwa ni Mei 3, 2020. Picha: Reuters/T. Mukoya

Shirika la Reli la Kenya lilisema mafuriko na maporomoko ya ardhi ya hivi karibuni yamesababisha ucheleweshwaji ambao haukutarajiwa wa mizigo kutoka Mombasa na Nairobi, pamoja na mizigo kufikishwa kwenye Bandari ya Mombasa.

Kulingana na shirika hilo, maporomoko hayo katika sehemu moja ya njia ya reli ya mizigo kati ya Mombasa na Nairobi yamesababisha kufungwa kwa sehemu hiyo kwa treni zote za mizigo, ingawa treni za abiria bado zinaendelea lakini kukiwa na ucheleweshaji.

Pembe ya Afrika imekumbwa na mvua kubwa na mafuriko yanayohusishwa na hali ya hewa ya El Nino katika wiki za hivi karibuni na kusababisha vifo vya karibu watu 46 nchini Kenya pekee.