1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

101110 Aung San Suu Kyi

Sekione Kitojo12 Novemba 2010

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar unajiandaa kumuachilia huru kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo.

https://p.dw.com/p/Q6x4
Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ibrahim Gambari akizungumza na Aung San Suu Kyi inchini Myanmar.Picha: picture-alliance/dpa

►Utawala wa kijeshi nchini Mynmar unajiandaa kumuchia huru hii leo kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Aung San Suu Kyi, kutoka kifungo cha nyumbani. Kiongozi huyo anaachiwa huru kufuatia uchaguzi wa bunge uliokipa ushindi wa asilimia 80 ya kura chama cha USDP, kilicho miongoni mwa vyama vilivyoundwa na utawala huo. Lakini suali linaloulizwa hivi sasa ni ikiwa utawala huo wa kijeshi utaviondoa vizuizi vilivyowekwa kuelekea nyumbani kwa Aung San Suu Kyi. ◄

Kuachiwa huru kwa Aung San Suu Kyi kunasubiriwa kwa hamu kubwa nchini Mynmar kufuatia kumalizika kwa uchaguzi wa bunge nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa rasmi utawala wa kijeshi umeanza matayarisho maalumu ya kumuachia kiongozi huyo mashuhuri wa upinzani. Msemaji wa utawala huo amesema mjini Rangon kwamba kuna mpango madhubuti wa usalama kwa ajili ya leo, siku ambapo kifungo cha Aung San Suu Kyi kinamalizika rasmi.

Aung San Suu Kyi, ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, ya mwaka 1992, kwa zaidi ya miaka 15 kati ya miaka 21 iliyopita, amekuwa gerezani au katika kifungo cha nyumbani. Mnamo mwaka 1990 aliongoza vuguvugu la demokrasia nchini Myanmar lililopata ushindi mkubwa katika uchaguzi, matokeo ambayo hayakutambuliwa na jeshi la nchi hiyo. Tangu wakati huo Aung San Suu Kyi amekuwa katika kifungo cha nyumbani, kwa sababu alitaka kufanyike mageuzi ya kidemokrasia nchini Myanmar. Hukumu yake ya mwisho aliipata wakati mwanamume mmoja raia wa Marekani alipoogelea hadi nyumbani kwake mjini Rangon, bila kibali.

Katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, mtoto wa kiume wa Aung San Suu Kyi, kwa jina Kim Aris, anasuburi visa ya kusafiria kwenda Myanmar. Kim ndiye mdogo kati ya watoto wawili wa kiume wa Aung San Suu Kyi. Hajamuona mamake tangu mwaka 1989. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 alirejea Myanmar akitokea nchini Uingereza, kwa lengo la kumuangalia mamake aliyekuwa akiugua. Wakati huo alianzisha vuguvugu la demokrasia, hadi wakati alipotupwa gerezani kwa mara ya kwanza, muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwaka 1990.

Kim Aris amesema hana uhakika kama atapewa visa ya kumuwezesha kusafiri kwenda Myanmar.

"Ubalozi hausemi lolote. Wanasema lazima watume ombi langu kwa wizara husika halafu wasubiri majibu. Watu hawa hawatabiriki. Ni vigumu kujua wanachofikiria. Ni vigumu kusema kama nitasafiri, lakini tutajua siku moja."

Kamati ya Nobel nchini Norway imefurahishwa sana na taarifa za kuachiwa huru kwa Aung San Suu Kyi. Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Noel hakuwa na fursa ya kusafiri mwaka 1992 kwenda mjini Oslo kupokea tuzo hiyo. Katibu wa kamati ya Nobel Geir Lundestad anasema.

O-ton Geir

"Bila shaka hizi zitakuwa habari njema sana kama ni kweli. Lakini kama ataachiwa huru, hatua nyengine inayopasa kufuata ni aruhusiwe kushiriki katika siasa. Sina matumaini kuhusu hilo kwa kuwa uchaguzi wa juzi haukuwa wa haki. Amekuwa katika kifungo cha nyumbani kwa karibu miaka 20 na hii ni aibu kubwa. Kwa hiyo juhudi zozote za kuiboresha hali yake zitakaribishwa."

Barabara za kuelekea nyumbani kwake Aung San Suu Kyi mjini Rangon bado zimefungwa kama ilivyokuwa hapo zamani. Katika kivuko cha kuingia barabara ya chuo kikuu, University Avenue, mjini humo ni watu wenye vibali pekee ndio wanaoruhusiwa kupita. Ikiwa vizuizi hivyo vitaondolewa mwishoni mwa juma hili baada ya kuachiwa huru kiongozi huyo, ni jambo la kusibiri na kuona.

Mwandishi: Josephat Charo7Brockamp, Mechthild/ Jablonski/ZPR

Mhariri: Aboubakar Liongo