Haki za binadamuNigeria
Amnesty yalishutumu jeshi la Nigeria kwa ukiukwaji wa haki
11 Juni 2024Matangazo
Ripoti ya shirika hilo imesema jeshi linaamini kuwa wasichana hao wanaliunga mkono kundi hilo la itikadi kali.
Katika taarifa yake jeshi limekanusha madai hayo, ambayo shirika la kutetea haki za binadamu limesema yalitokana na mahojiano yaliyofanywa mwaka 2019 hadi 2024 na wanawake126 ambao zamani walikuwa mateka. Wahanga 31 wamesema walishikiliwa kinyume cha sheria katika kambi za jeshi kwa siku kadhaa hadi karibu miaka minne kati ya mwaka 2015 hadi katikati ya mwaka 2023.
Ripoti hiyo inasema hatua hiyo ilitokana na dhana au misimamo yao kuhusu kundi la Boko Haram. Umoja wa Mataifa umesema kundi la Boko Haram limewaua zaidi ya watu 35,000.