1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini yawatimua Walibya 95 waliokuwa kizuizini

18 Agosti 2024

Wizara ya mambo ya ndani nchini Afrika Kusini imesema raia 95 wa Libya waliopatikana katika kambi ya kijeshi inayoshukiwa kuwa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo mwezi Julai wamefukuzwa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4jbLp
Afrika Kusini
Polisi nchini Afrika ya Kusini waliwashuku raia wa Libya kuwa wanafanya mazoezi ya kijeshiPicha: Stringer/AFP/Getty Images

Wizara ya mambo ya ndani nchini Afrika Kusini imesema raia 95 wa Libya waliopatikana katika kambi ya kijeshi inayoshukiwa kuwa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo mwezi Julai wamefukuzwa nchini humo.

Wanaume hao wa Libya wamezuiliwa tangu Julai 26 wakati polisi walipovamia kambi ya mafunzo iliyopo karibu na mji wa White River umbali wa takribani kilomita 360 mashariki mwa Johannesburg.

Soma zaidi. SADC: Watu milioni 68 wanakabiliwa na athari za ukame

Polisi walisema watu hao waliingia Afrika Kusini mwezi Aprili kwa viza zilizotolewa kwa ajili ya mafunzo kama walinzi, lakini polisi waliwashuku kupatiwa mafunzo ya kijeshi.

Hapo awali, kundi hilo lilikuwa limeshtakiwa kwa kukiuka sheria za uhamiaji ambapo kesi yao iliahirishwa kwa uchunguzi zaidi, lakini siku ya Alhamisi kesi hiyo ilitupiliwa mbali na Mamlaka ya Kitaifa ya Mashtaka ya Afrika Kusini kwa kutokuwa na ushahidi wa kutosha.