Mshukiwa wa ujangili akamatwa Afrika Kusini
14 Agosti 2024Matangazo
Nyama hiyo mara nyingi imekuwa ikisafirishwa kwa magendo kuelekea Asia. Mshukiwa huyo alikuwa na mabegi 27 ya plastiki yaliyokuwa na zaidi ya chaza elfu 13,000 wenye uzito wa kilo 640.
Wizara ya mazingira imetoa wito wa kufunguliwa mashtaka haraka dhidi ya mshukiwa huyo, ambaye alikamatwa wiki iliyopita. Mtu huyo alitiwa mbaroni wakati wa msako wa polisi huko Eastern Cape, mkoa wenye mwambao mrefu katika bahari ya Hindi.
Kilo moja ya chaza mkavu inaweza kuwa na thamani ya hadi randi 6,000 sawa na dola 330 za Kimarekani. Kiwango cha chaza kinachosafirishwa kimagendo kimeongezeka maradufu katika muongo mmoja uliopita, kulingana na mtandao wa ufuatiliaji wa biashara ya wanyamapori na viumbe wa baharini, TRAFFIC.