1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky amshukuru Kansela Scholz katika mazungumzo yao

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na kumshukuru kwa usaidizi muhimu wa kiulinzi.

https://p.dw.com/p/4mxYj
Scholz na Zelenskyj
Kansela wa Ujeruman Olaf Scholz na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Picha: abaca/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyyamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na kumshukuru kwa usaidizi muhimu wa kiulinzi pamoja na uongozi wake wa kuwaunganisha washirika muhimu katika uungaji mkono Ukraine. Ujerumani yaahidi msaada zaidi wa silaha kwa Ukraine

Aidha, Rais Zelensky ameeleza kuwa Kansela Scholz amethibitsha ya kwamba mfumo wa ulinzi wa anga wa IRIS-T utawasilishwa Ukraine mwishoni mwa mwaka huu. Zelensky ameandika kupitia mtandao wa X, akielezea matumaini yake kwamba msaada wa Ujerumani kwa Kiev utaendelea, licha ya kuanguka kwa serikali ya mseto ya Ujerumani na uchaguzi wa mapema uliopangwa Februari 23.Scholz asisitiza kuhusu mazungumzo ya amani kwa Ukraine

Wakati hayo yakijiri, jeshi la anga la Ukraine limetangaza hali ya tahadhari ya nchi nzima kufuatia mashambulizi mengi ya makombora ya Urusi na droni ikiwemo katika mji mkuu wa Kiev na maeneo mengine.